• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais John Magufuli aomba kuchaguliwa tena kuwa rais

    (GMT+08:00) 2020-06-18 10:12:47

    Rais John Magufuli wa Tanzania amechukua fomu ya kugombea urais kwa muhula wa pili. .

    Katibu mkuu wa Chama tawala cha Mapinduzi (CCM) Bw. Bashiru Ally alimkabidhi fomu Bw. Magufuli katika makao makuu ya CCM, mkoani Dodoma.

    Taarifa iliyotolewa na Ikulu ya Tanzania imesema Rais Magufuli amewataka wanachama wa CCM na watanzania kumuunga mkono katika safari yake ya kuwa mgombea wa chama hicho katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba.

    Aidha rais Magufuli amewahimiza wanachama wa chama hicho kushiriki katika mchakato wa uchaguzi kwa amani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako