• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mwanataaluma wa Tanzania asema mamlaka ya China inapaswa kuheshimiwa

    (GMT+08:00) 2020-06-18 10:21:21

    Gazeti la Tanzania Mwananchi tarehe 16 Juni lilitoa Makala iliyoandikwa na mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaamu Bw. Darius Mukiza "Mamlaka ya China inapaswa kuheshimiwa".

    Kwenye makala hiyo Bw. Mukiza amesema, ili kulinda mamlaka, usalama na maslahi ya maendeleo ya nchi, kulinda sera ya "Nchi Moja, Mifumo Miwili", kuhakikisha amani na usalama wa kudumu wa Hongkong na maslahi na haki ya wakazi wa huko, tarehe 28 Mei, Bunge la Umma la China lilipitisha azimio kuhusu kujenga na kukamilisha mfumo wa sheria na utaratibu wa utekelezaji wa kulinda usalama wa taifa katika Mkoa wenye Utawala Maalum wa Hong Kong. Lakini Marekani, Uingereza, Canada na Australia zilitoa taarifa ya pamoja kudai kuwa hatua hii ya China imeharibu sera ya "Nchi Moja, Mifumo Miwili", kuathiri vibaya hadhi ya Hongkong ya kujitawala, na maendeleo na ustawi wake. Marekani imepanga kutunga sheria ya kufuta hadhi maalumu ya Hongkong, Uingereza pia imetishia kutoa haki nyingi zaidi za uhamiaji kwa wakazi wa Hongkong wenye pasipoti ya "wananchi wa Uingereza wanaoishi nchi za ng'ambo".

    Amesema "Nchi Moja, Mifumo Miwili" ni mwongozo wa kimsingi wa serikali kuu ya China katika mkoa wa Hongkong. China kama nchi nyingine yenye mamlaka kamili, kamwe haitavumilia kitendo chochote cha kuifarakanisha nchi, au kuvamia madaraka ya serikali kuu kwa kisingizio cha kutafuta "uhuru wa Hongkong" .

    Mwaka jana vurugu zilitokea mkoani Hongkong, baadhi ya watu wenye siasa kali kushambulia Mamlaka ya serikali kuu huko Hongkong, kudhalilisha bendera na nembo ya taifa, vitendo ambavyo viliwakasirisha wachina wote duniani. Mbali na hayo, Marekani pia ilitangaza "Sheria ya haki za binadamu na demokrasia ya Hongkong", kuingilia kimabavu mambo ya ndani ya China. Kutokana na hali hii, China ina ulazima na uharaka wa kutunga sheria ya kuhakikisha usalama wa taifa mkoani Hongkong.

    Amesisitiza kuwa kwa nchi yoyote duniani, utungaji wa sheria kuhusu usalama wa taifa ni madaraka ya kutunga sheria. Kifungu nambari 23 kwenye sheria za kimsingi za Hongkong ni mpango maalumu uliowekwa kwa kufuata sera ya "Nchi Moja, Mifumo Miwili", ambacho hakiwezi kubadilisha ukweli kwamba madaraka ya kutunga sheria kuhusu usalama wa taifa yanamilikiwa na serikali kuu, na nchi nyingine hazina haki ya kuingilia kati.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako