• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ikulu ya Kenya yatoa taarifa ya "China kuahidi kushirikiana na Afrika katika mapambano dhidi ya Virusi vya Corona"

    (GMT+08:00) 2020-06-18 10:25:57

    Ikulu ya Kenya imetoa taarifa ya "China kuahidi kushirikiana na Afrika katika mapambano dhidi ya Virusi vya Corona", kufuatia matokeo yaliyotolewa kwenye mkutano maalumu wa Mshikamano na Ushirikiano katika kupambana na COVID-19 uliofanyika jana.

    Rais Uhuru Kenyatta ameishukuru China kwa mwitikio wa haraka na kutoa vifaa tiba ikiwemo vitendanishi, vifaa vya kujikinga na dawa kwa Kenya na bara zima la Afrika. Amesema hatua hiyo siyo tu imeisaidia Kenya kupambana na virusi vya Corona bali pia imeisaidia Kenya kupambana na maafa ya nzige.

    Taarifa hiyo inasema, dhamiria ya China ya kuimarisha mshikamano na ushirikiano kati yake na Afrika haitabadilika, itaendelea kutoa uungaji mkono wa kiufundi na vifaa vinavyohitajika kwa Afrika. Baada ya China kutoa chanjo ya virusi vya Corona, itazinufaisha nchi za Afrika kwanza. Taarifa pia imesema China na Afrika zitashikamana kushikilia taratibu za pande nyingi, kupinga kufanya janga la virusi vya Corona kuwa silaha ya kisiasa na kuihuisisha China na virusi hivyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako