• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yapinga vikali muswada wa Marekani kuhusu Xinjiang

    (GMT+08:00) 2020-06-18 19:36:30

    Wizara ya mambo ya nje ya China imetoa taarifa ikipinga vikali muswada wa Marekani kuhusu Wauyghur wa China, na kusema unapaka matope hali ya haki za binadamu ya mkoa wa Xinjiang, China.

    Taarifa hiyo imesema muswada huo umeharibu sera ya usimamizi ya China, kuingilia mambo ya ndani ya China na kwenda kinyume na sheria ya kimataifa na kanuni za uhusiano wa kimataifa.

    Wizara hiyo imesema, suala la Xinjiang si suala la haki za binadamu, kikabila au kidini bali ni suala la kupinga ugaidi na ufarakanishaji, na kuongeza kuwa, Xinjiang iliathiriwa vibaya na msimamo mkali, vitendo vya kigaidi na kiufarakanishaji, ambavyo vilitishia sana usalama wa mali na maisha ya watu wa huo.

    Wizara hiyo pia imesema, haipaswi kupima jitihada za kupambana na ugaidi kwa vigezo tofauti, muswada wa Marekani haujali hali halisi, na unalenga kuchochea uhusiano wa kikabila wa China, kuharibu ustawi na utulivu wa Xinjiang na kuzuia maendeleo ya China.

    Bunge la umma na baraza la mashauriano ya kisiasa la China siku hiyo pia yamelaani mswada huo wa Marekani.

    Shirika Kuu la Utangazaji la China CMG leo pia limetoa tahariri, likiona kuwa Marekani itajiumiza kutokana na kuunga mkono magaidi kwa kisingizio cha haki za binadamu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako