• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Rwanda asifu China kwa kutoa misaada ya dharura kwa Afrika

    (GMT+08:00) 2020-06-18 19:36:44

    Rais Paul Kagame wa Rwanda ameisifu China kwa misaada yake kwa nchi za Afrika katika mapambano yao dhidi ya virusi vya Corona, na kuishukuru kwa ahadi yake ya kutoa misaada yenye thamani ya dola za Marekani bilioni 2 ndani ya miaka miwili.

    Ikulu ya Rwanda imetoa hotuba ya rais Kagame aliyoitoa kwenye mkutano maalum wa mshikamano wa China na Afrika katika mapambano dhidi ya virusi vya Corona uliofanyika jana kwa njia ya video.

    Rais Kagame amesema, katika kipindi hiki kigumu, mshikamano huo umeonesha tena mafanikio yaliyopatikana katika Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika. Amesema serikali na watu wa China wametoa misaada na kusafirisha vifaa muhimu vya matibabu katika kipindi hicho ambapo Afrika inahitaji zaidi misaada.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako