• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China atoa salamu kwa mkutano wa ushirikiano wa kimataifa wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja"

    (GMT+08:00) 2020-06-19 07:37:03

    Mkutano wa ngazi ya juu wa ushirikiano wa kimataifa wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja" umefanyika leo hapa Beijing.

    Katika salamu zake kwa mkutano huo, Rais Xi Jinping wa China amesema, China inapenda kushirikiana na nchi nyingine kujenga jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja. Amesema maambukizi ya virusi vya Corona yametambulisha kuwa, hatma za nchi mbalimbali duniani zinahusiana kwa karibu, na kushinda virusi hivyo na kufufua uchumi kunahitaji mshikamano na ushirikiano.

    Amesisitiza kuwa China siku zote inashikilia kujiendeleza kwa njia ya amani na kunufaishana na pande nyingine, na inapenda kushirikiana na nchi nyingine kujenga "Ukanda Mmoja, Njia Moja" kuwa njia ya ushirikiano, afya, kufufua uchumi, na kuongeza uwezo wa kupata maendeleo.

    Mkutano huo umeandaliwa na wizara ya mambo ya nje, wizara ya biashara, kamati kuu ya maendeleo na mageuzi na kamati ya afya ya China, ukiwa na kauli mbiu ya "Kuimarisha ushirikiano wa kimataifa wa 'Ukanda Mmoja, Njia Moja': Kushirikiana kukabiliana na COVID-19."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako