• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kuendeleza ushirikiano wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja" licha ya athari za COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-06-19 08:12:12

    Serikali ya China imetangaza kuwa itaendeleza zaidi ushirikiano wa kimataifa chini ya pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" licha ya athari za janga la COVID-19.

    Mjumbe wa taifa wa China na waziri wa mambo ya nje Bw. Wang Yi aliongoza mkutano wa ngazi ya juu kuhusu ushirikiano wa kimataifa wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja" uliofanyika kwa njia ya video hapa Beijing, ambao ulianza na hotuba ya maandishi iliyotolewa na rais Xi Jinping.

    Waziri Wang Yi alisisitiza msimamo wa rais Xi juu ya kusukuma mbele maendeleo ya pamoja yenye ubora na kuhimiza taratibu za pande nyingi na wenzi wa "Ukanda Moja, Njia Moja" ili kulinda afya ya watu na kufufua uchumi wa dunia wakati wa kukabiliana na janga la virusi vya Corona.

    Mawaziri kutoka nchi 25, pamoja na wawakilishi kutoka Umoja wa Mataifa na Shirika la Afya Duniani WHO, wameshiriki kwenye mkutano huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako