• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mpango wa Nigeria wa kufungua tena viwanja vya ndege wakumbwa na changamoto nyingi

    (GMT+08:00) 2020-06-19 09:32:32
    Mpango wa Nigeria wa kufungua tena viwanja vya ndege tarehe 21 mwezi Juni umecheleweshwa kutokana na vikwazo vingi vilivyopo kwenye sekta ya usafiri wa anga wakati nchi hiyo inajitahidi kutatua changamoto zilizosababishwa na janga la COVID-19.

    Baraza la Seneti la Nigeria limesema baada ya mkutano kati ya watunga sheria na wafanyakazi wa sekta ya usafiri wa anga kwamba kutokana na hali iliyopo, mpango wa kufungua tena viwanja vya ndege kwa sasa ni mgumu.

    Wawakilishi wa wafanyakazi wa sekta ya anga wamesema katika mkutano huo kwamba uingiliaji maalum wa kifedha na utoaji wa itifaki muhimu na mifumo ya kinga vinahitajika kwa kuzingatia janga la COVID-19 kabla ya kufungua tena viwanja vya ndege.

    Kwa upande mwingine, mtaalam wa afya ya umma wa Zambia Bw. Rhoda Nchinga amesema ni nzuri kuwahimiza watu kudumisha miendendo ya usafi inayotekelezwa wakati wa janga la COVID-19, ambayo inasaidia kuzuia mlipuko mwingine wa magonjwa.

    Hivi sasa katika mji mkuu wa Zambia Lusaka, maeneo ya umma kama shule, vituo vya mabasi na sehemu za biashara vina vituo vya kunawa mikono vinavyokusudiwa kuhamasisha umma kudumisha mazoea mazuri ya kiafya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako