• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatoa misaada ya vifaa tiba kwa Sudan na Guinea-Bissau

    (GMT+08:00) 2020-06-19 09:58:53

    Serikali ya China imetoa shehena nyingine ya vifaa tiba kwa Sudan ili kuongeza juhudi zake katika kupambana na janga la COVID-19.

    Balozi wa China nchini Sudan Bw. Ma Xinmin amesema China na Sudan ni marafiki wa karibu na washirika wa kimkakati, ambao kwa miaka mingi wameungana mkono na kusaidiana, na wako bega kwa bega katika mapambano dhidi ya janga la COVID-19.

    Kwa upande wake, waziri wa mambo ya nje wa Sudan Bw. Omer Gamar-Eddin amewashukuru watu na serikali ya China kwa ushirikiano na Sudan, na anatumai kuwa ushirikiano huo utaendelea katika nyanja nyingine.

    Wakati huohuo shehena ya pili ya msaada wa vifaa tiba kutoka serikali ya China umewasili nchini Guinea-Bissau kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Ossado Vieira.

    Kamishna mkuu wa mapambano dhidi ya janga la COVID-19 wa Guinea-Bissau Dr. Magda Robalo Correia e Silva ameishukuru serikali ya China, na kusema China ni nchi rafiki wa wakati wote wa Guinea-Bissau.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako