Ofisi ya Shirika la Afya Duniani WHO barani Ulaya imetoa tahadhari ikeeleza kuwa ongezeko la idadi ya wagonjwa wa COVID-19 katika eneo la Ulaya Mashariki linaleta wasiwasi, ingawa idadi hiyo inazidi kupungua katika nchi nyingine za Ulaya katika wiki kadhaa zilizopita.
Mkurugenzi wa ofisi hiyo Dkt Hans Kluge amesema katika mwezi uliopita, idadi ya nchi za Ulaya zilizokumbwa na ongezeko la wagonjwa wa virusi hivyo imeongezeka kutoka 6 hadi 21.
Dkt Kluge amesema kuweka zuio la usafiri na kudumisha umbali wa kijamii kunasaidia, lakini hatari bado iko juu kote duniani.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |