• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ofisa wa Ethiopia apongeza ushirikiano na China katika sekta ya teknolojia ya kidigitali

    (GMT+08:00) 2020-06-19 10:37:05

    Ofisa wa Ethiopia amepongeza ushirikiano wa kidigitali ulioanzishwa kati ya nchi yake na China, wakati nchi hiyo ikifanya juhudi kuchochea uchumi kufuatia mlipuko wa virusi vya Corona.

    Msemaji wa waziri mkuu wa Ethiopia Bi Benene Seyoum amesema, mapema ya mwezi huu, Ethiopia imepitisha mkakati wa kwanza wa kidigitali wa nchi hiyo, huku akisema msaada wa kiteknolojia kutoka China unakaribishwa.

    Bi Seyoum amesema baraza la mawaziri la nchi hiyo limepitisha mkakati wa kwanza wa kidigitali, na kuona kwamba huduma na mikakati mingi imekuwa ya kidigitili wakati wa kupambana na virusi vya Corona.

    Ameongeza kuwa kuzindua uchumi wa kidigitali kwa nchi hiyo ni sehemu ya mkakati mkubwa wa kiuchumi wa nchi hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako