• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Shirikisho kuu la Wafanyabiashara wa Afrika mkoani Guangdong lashiriki kwenye maonyesho ya 127 ya biashara ya Guangdong

    (GMT+08:00) 2020-06-19 19:18:37

    Shirikisho kuula Wafanyabiashara wa Afrika mkoani Guangdong, China limefanya mkutano na matawi yake wakati wa maonyesho ya 127 ya biashara ya Guangdong yaliyoanza jumatatu wiki hii kwa njia ya mtandao wa Internet, na kusema litawahimiza wafanyabiashara wa Afrika washiriki kwenye maonesho hayo.

    Wajumbe wa Shirikisho hilo wameeleza imani yao kuhusu maonyesho hayo na ushirikiano wa biashara kati ya China na Afrika, na kusema wanapenda kusukuma mbele kwa pamoja utekelezaji wa biashara ya mtandao kwenye maonyesho hayo.

    Shirikisho hilo limesema, maonyeshao hayo yanatoa fursa kwa makampuni ya Afrika kuona na kuagiza bidhaa, na kutembelea viwanda vya kuzalisha bidhaa hizo kupitia mtandao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako