• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Chanjo za COVID-19 huenda zitatolewa kabla ya mwisho wa mwaka huu

    (GMT+08:00) 2020-06-19 19:32:00

    Mwanasayansi mwandamizi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Dr. Soumya Swaminathan amesema, mpaka sasa kuna chanjo zisizopungua 200 za virusi vya Corona (COVID-19) zinazofanyiwa utafiti.

    Amesema chanjo 10 zimefanyiwa majaribio ya kliniki, na chanjo 3 zinatarajiwa kufaniwa majaribio ya kipindi cha mwisho, zikiwemo chanjo kutoka China.

    Dr Swaminathan amesema, matokeo ya majaribio ya kwanza na ya pili ya chanjo kadhaa za China yalionesha mafanikio, na anatarajia kuwa hadi kufikia mwaka 2021, chanjo bilioni 2 zitatengenezwa. Dr. huyo ameongeza kuwa, mabadiliko ya jeni za virusi vya Corona ni madogo kuliko virusi vya mafua, na sehemu za kiini zilizosababisha ugonjwa mbaya na majibu ya kinga bado hazijakuwa na mabadiliko.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako