• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wataalamu wa Afrika wapongeza Mkutano wa Kilele wa China na Afrika dhidi ya COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-06-19 20:13:42

    Mkutano wa Kilele wa Mshikamano na Ushirikiano kati ya China na Afrika katika kupambana na COVID-19 ulifanyika tarehe 17 mwezi huu, na umesifiwa sana na wanasiasa, wataalamu na wasomi wa nchi mbalimabli za Afrika.

    Taarifa iliyotolewa na Ikulu ya Kenya imesema, China na Afrika zinashikamana na kushikilia utaratibu wa pande nyingi, huku zikipinga kulifanya janga hilo liwe suala la kisiasa.

    Mwenyekiti wa Shirikisho la ushirikiano na maendeleo kati ya Afrika na China la Morocco Bw. Nasser Bouchiba amesema, mkutano huo umeonyesha ushirikiano wa sekta ya afya kati ya pande hizo unainuka, ambao ni muhimu zaidi katika ujenzi na marekebisho ya mfumo wa afya ya umma wa nchi za Afrika.

    Mwanadiplomasia wa zamani wa wizara ya uhusiano na ushirikiano wa kimataifa nchini Afrika Kusini Bw. Gert Grobler amesema mkutano huo umethibitisha uhusiano wa ushirikiano wa karibu kati ya China na Afrika. Amesema pande hizo zinaweza kufanya ushirikiano wa kiujenzi, utakaosaidia kujenga jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako