• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda yakumbwa na kukatika kwa umeme bila chanzo kujulikana

    (GMT+08:00) 2020-06-22 07:55:46

    Shirika la umeme la Uganda limetangaza kuwa jana Uganda ilikumbwa na kukatika umeme katika nchi nzima, lakini chanzo cha kukatika huko hakijajulikana.

    Taarifa iliyotolewa na shirika hilo imesema uchunguzi ulikuwa unaendelea kubaini chanzo cha tukio hilo. Hii si mara ya kwanza kwa tukio kama hili kutokea nchini Uganda, tarehe 9 mwezi Mei tukio kama hili lilitokea na sababu yake haikujulikana. Tarehe 4 Aprili kulikuwa na kukatika umeme tena baada ya magugu maji kwenye eneo la ekari 12 kuathiri kituo cha kuzalisha umeme kwa maji cha Nalibale, kaskazini mwa Jinja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako