• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Libya inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa yalaani kauli ya rais wa Misri kuwa "tangazo la vita"

    (GMT+08:00) 2020-06-22 07:56:05

    Serikali ya Libya inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa inachukulia kauli iliyotolewa na Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi kuwa ni "tangazo la vita".

    Taarifa iliyotolewa na serikali hiyo imesema Libya inachukulia uingiliaji wa mambo yake ya ndani na ukiukaji wa mamlaka yake, hata kama ni kwa njia ya taarifa kupitia vyombo vya habari, kama ilivyotolewa na Rais wa Misri, au kuunga mkono mapinduzi au mamluki, kuwa havikubaliki na vinachukuliwa kama kitendo cha uhasama, na tangazo la vita.

    Taarifa pia imeonya kuhusu matokeo ya uingiliaji wa mambo ya ndani ya Libya, kuwa utasababisha madhara makubwa na kuyumbisha kanda nzima.

    Jumamosi Rais al-Sisi alitangaza utayari wa jeshi la Misri kuingilia na kuisaidia Libya dhidi ya magaidi na makundi yenye silaha.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako