• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania kujenga zaidi ya 300 ya miradi mipya ya umwagiliaji ndani ya miaka 5

    (GMT+08:00) 2020-06-22 08:18:49

    Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Tanzania jana imesema, imepanga kujenga miradi 384 ya kilimo cha umwagiliaji yenye thamani ya shilingi bilioni 986.8 (karibu dola za kimarekani milioni 426) nchini kote katika miaka mitano ijayo.

    Kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika huko Dodoma, mkurugenzi wa tume hiyo Bw. David Kaali amesema miradi hiyo mipya itajengwa kwenye mikoa ya Dodoma, Kilimanjaro, Mbeya, Morogoro, Mtwara, Mwanza, Tabora na Katavi.

    Bw. Kaali amesema fedha za ujenzi wa miradi hiyo zitapatikana chini ya utekelezaji wa kipindi cha pili cha Mpango wa Maendeleo ya Sekta ya Kilimo. Vilevile amesisitiza kuwa miradi hiyo mipya itasaidia kuimarisha usalama wa chakula nchini Tanzania.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako