• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tukio la shambulizi la kisu nchini Uingereza latangazwa kuwa la kigaidi

    (GMT+08:00) 2020-06-22 16:54:55

    Polisi wa Idara ya kupambana na ugaidi nchini Uingereza imesema, tukio la shambulizi la kisu lililotokea katika mji Reading Jumamosi usiku kwa sasa limetangazwa kuwa la kigaidi.

    Watu watatu waliuawa na wengine watatu kujeruhiwa katika shambulizi lililofanywa kwenye bustani ya Forbury huko Reading Jumamosi usiku, na mwanaume mmoja mkazi wa Reading amekamatwa katika eneo la tukio kwa tuhuma za kuhusika na mauaji hayo.

    Shirika la Habari la BBC limeripoti kuwa, mwanaume huyo aliyetambuliwa kwa jina la Khairi Saadallah asili yake ni nchini Libya.

    Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson ameeleza kusikitishwa na kuhuzunishwa na shambulizi hilo, na kupongeza ujasiri wa polisi ambao hawakuwa na silaha waliofanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako