• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nigeria kuongeza ushirikiano wa Ukanda Mmoja na Njia Moja na China baada ya mlipuko wa COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-06-22 17:20:02

    Msemaji wa rais wa Nigeria Bw. Garba Shehu amesema, nchi hiyo inatarajia kuongeza ushirikiano na China katika ujenzi wa "Ukanda Mmoja na Njia Moja" baada ya kumalizika kwa mlipuko wa virusi vya Corona.

    Bw. Shehu amesema, baada ya mlipuko huo kutokea barani Afrika, China imechukua hatua halisi kuzisaidia nchi za bara hilo kupambana na virusi hivyo na kuonesha majukumu ya nchi kubwa. China imetoa vifaa vya matibabu, kutuma vikosi vya madaktari na kufanya mikutano kwa njia ya video na wataalam wa matibabu wa Afrika ili kubadilishana uzoefu wa kupambana na virusi hivyo.

    Pia amesema, Nigeria imefanya ushirikiano mzuri na China chini ya pendekezo la "Ukanda Mmoja na Njia Moja", na inaikaribisha China kuongeza uwekezaji nchini humo na kutarajia kupanua ushirikiano na China katika sekta ya viwanda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako