• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mapigano nchini Afghanistan yaendelea kuwa mbaya

    (GMT+08:00) 2020-06-22 19:04:40

    Mapigano nchini Afghanistan yameongezeka katika siku mbili zilizopita, wakati mazungumzo ya amani kati ya serikali ya nchi hiyo na kundi la Taliban yakikaribia kufanyika huko Qatar.

    Msemaji wa polisi wa mkoa wa Kapisa, Bw. Shaeq Shurash amesema, katika mapambano ya hivi karibuni, kundi la Taliban limeshambulia kituo cha ukaguzi cha polisi wilayani Nijrab na kusababisha vifo vya askari polisi wawili na mwingine mmoja kujeruhiwa.

    Habari zinasema, kundi la Taliban limefanya mashambulizi 422 katika mikoa 32 katika wiki iliyopita na kusababisha vifo vya askari 291 wa vikosi vya usalama, na wengine 550 kujeruhiwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako