• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Afrika Kusini aonya dhidi ya kupunguza wafanyakazi wakati nchi hiyo ikikabiliwa na mlipuko wa virusi vya Corona

    (GMT+08:00) 2020-06-22 19:07:00

    Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini amezitaka kampuni zinazopanga kupunguza wafanyakazi ili kudumisha utulivu wa biashara na maisha ya wafanyakazi licha ya kuathiriwa vibaya na virusi vya Corona kuacha kutekeleza mpango huo.

    Katika hotuba yake ya kila wiki kwa taifa hilo, rais Ramaphosa amesema ingawa nchi hiyo inajitahidi kulinda ajira zilizopo na kuanzisha ajira nyingine mpya, pia kuvutia ngazi mpya ya uwekezaji. Amesisiza umuhimu wa kufungua nyanja mpya kwa ajili ya ujasiriamali na kujiajiri, hususan kwa vijana.

    Rais Ramaphosa amesema hayo baada ya kampuni kadhaa wiki iliyopita kutangaza mpango wa kupunguza wafanyakazi kutokana na hasara kubwa waliyopata katika miezi mitatu iliyopita.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako