• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yasisitiza kuwa inashughulikia kesi kuhusu wananchi wa Canada kwa kufuata sheria

    (GMT+08:00) 2020-06-22 19:12:40

    Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bw. Zhao Lijian amesisitiza kuwa, idara ya sheria ya China itashughulikia kesi inayowahusu raia wawili wa Canada kwa uhuru, na pia itahakikisha haki halali ya wananchi wa Canada kwa kufuata sheria.

    Zhao amesema hayo alipojibu maswali kuhusu China kuwakamata na kuwafungulia mashitaka raia wawili wa Canada Michael Kovrig na Michael Spavor, kitendo ambacho kinachukuliwa na baadhi ya watu kuwa ni kulipiza kisasi kwa China dhidi ya kesi ya Bibi Meng Wanzhou.

    Bw. Zhao amesema, hivi karibuni kauli zenye makosa zilizotolewa na Canada zimeonesha kuwa, Canada inachukua vigezo viwili juu ya suala la "uhuru wa sheria". Raia hao wawili wa Canada walikamatwa kwa tuhuma za kuharibu usalama wa China. Amesema China inawahimiza viongozi wa Canada kuheshimu utawala wa kisheria, na sheria na mamlaka ya China, na kusimamisha kutoa kauli zisizowajibika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako