• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wataalamu wa WHO wasema COVID-19 umejikita kote duniani

    (GMT+08:00) 2020-06-23 08:41:00

    Mkurugenzi mtendaji wa Mipango ya Dharura wa Shirika la Afya Duniani WHO Bw. Michael Ryan, amesema kutokana na kuongezeka kwa kasi ya maambukizi hasa kwenye baadhi ya nchi zenye idadi kubwa ya watu, mlipuko wa virusi vya Corona sasa umejikita kote duniani.

    Bw. Michael Ryan amesema mlipuko wa COVID-19 unaelekea kileleni katika baadhi ya nchi kubwa kwa wakati mmoja, hali inayochangia ongezeko kubwa la maambukizi duniani.

    Hadi kufikia Jumapili idadi ya maambukizi mapya ya COVID-19 kote duniani imezidi 183,000, ambalo ni ongezeko kubwa zaidi kwa siku tangu virusi vya Corona vilipuke.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako