• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Katibu mkuu wa UM aeleza wasiwasi kuhusu usalama wa raia kaskazini magharibi mwa Syria

    (GMT+08:00) 2020-06-23 08:41:21

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres ameeleza wasiwasi wake juu ya usalama wa raia zaidi ya milioni nne walioko kaskazini magharibi mwa Syria, kufuatia mashambulizi ya anga na mizinga yaliyoripotiwa wikiendi, ambayo yameathiri maeneo 14 katika mikoa ya Idlib na Hama.

    Msemaji wa katibu mkuu huyo Bw. Stephane Dujarric amesema Umoja wa Mataifa unaendelea kuzihimiza pande zote, na wale wenye ushawishi kwa pande hizo, kuhakikisha ulinzi wa raia na miundombinu ya kiraia, kulingana na wajibu wao chini ya sheria ya kibinadamu ya kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako