• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Afrika wasema COVID-19 inahatarisha afya, usalama na uchumi wa Afrika

    (GMT+08:00) 2020-06-23 09:02:05

    Umoja wa Afrika umesema mlipuko wa ugonjwa wa COVID-19 barani Afrika umeleta hatari kubwa kwa mazingira ya afya, usalama na usalama na mambo ya kiuchumi na kijamii.

    Taarifa iliyotolewa jana na Umoja wa Afrika imesisitiza kuwa chanjo ndio njia yenye ufanisi zaidi na Afrika inatakiwa kushiriki kikamilifu kwenye utengenezaji wa chanjo, majaribio ya kimatibabu, na kushughulikia mambo yanayohusu upatikanaji wa chanjo hiyo. Taarifa pia imesema chanjo yenye ufanisi itaokoa maisha na uchumi, na kufanya hali irudi kuwa ya kawaida hatua kwa hatua barani Afrika na dunia nzima.

    Mwezi Februari mwaka huu Umoja wa Afrika ulitunga mkakati wa pamoja wa kupambana na virusi vya Corona ukiwa na nguzo tatu kuu yaani kudhibiti maambukizi, kuzuia vifo na kupunguza madhara yake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako