• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkuu wa ulinzi wa amani wa UM asema hali ya kisiasa nchini CAR bado ni tete

    (GMT+08:00) 2020-06-23 09:03:02

    Hali ya kisiasa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati inaendelea kuwa tete huku ikigubikwa na maandalizi ya uchaguzi wa rais na wabunge uliopangwa kufanyika mwezi Desemba mwaka huu.

    Akiongea kuhusu hali hiyo naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia operesheni za kulinda amani Bw. Jean Pierre Lacroix, amesema makundi yenye silaha ikiwa ni pamoja na makundi yaliyosaini makubaliano ya amani, yote yanatambua mwito wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa wa kuacha mapambano, lakini bado yanaendelea kutumia silaha kwa malengo ya kupanua maeneo yake.

    Bw. Lacroix amelaani vikali shambulizi lililotokea jumapili dhidi ya tume ya pamoja ya doria ya Umoja wa mataifa na Mali, lililofanywa na kundi la Retour lililosaini makubaliano ya amani mwezi Februari.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako