• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda yatangaza bajeti ya dola bilioni 3.5 za Kimarekani kujenga ustahimilivu wa uchumi

    (GMT+08:00) 2020-06-23 09:25:20

    Rwanda Jumatatu ilitangaza bajeti mwaka 2020 na 2021 ya dola bilioni 3.5 za Kimarekani kwa ajili ya kujenga ustahimilivu wa uchumi kufuatia athari za janga la COVID-19.

    Waziri wa fedha wa nchi hiyo Bw. Uzziel Ndagijimana, amesema moja ya vipaumbele vya bajeti hiyo ni kufufua biashara zinazoathiriwa na janga hilo, na nyanja nyingine ni pamoja na kuimarisha mfumo wa afya kwa kuongeza upatikanaji wa huduma bora za afya kwa watu wote, kuongeza tija kwenye sekta ya kilimo na ufugaji, na kuhimiza sera ya "Made in Rwanda" ili kupunguza nakisi ya biashara na kujenga ustahimilivu wa uchumi.

    Aidha bajeti hiyo pia itazingatia kuendeleza miundombinu na teknolojia za kidijitali, ili kuboresha utoaji wa huduma, kuongeza upatikanaji wa elimu yenye ubora, kutokomeza utapiamlo na hali ya kudumaa kwa watoto, kuimarisha utayari na uwezo wa kushughulikia majanga, na kuongeza ajira kupitia uwekezaji katika miundombinu ya umma.

    Bw. Ndagijimana amesema asilimia 60.7 ya bajeti hiyo itatokana na vyanzo vya ndani vya mapato, na nyingine asilimia 39.3 ni ufadhili kutoka nje.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako