• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baraza la haki za binadamu la UM lapitisha azimio lililotolewa na China kuhusu ushirikiano wa kunufaishana kati ya pande nyingi

    (GMT+08:00) 2020-06-23 09:28:13

    Baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa limepitisha azimio lililotolewa na China kuhusu kuimarisha ushirikiano wa kunufaishana kati ya pande nyingi kwenye sekta ya haki za binadamu.

    Azimio hilo liitwalo "Kuimarisha ushirikiano wa kunufaishana kati ya pande nyingi kwenye sekta ya haki za binadamu", limesisitiza umuhimu wa kuhimiza uhusiano wa kimataifa kwa msingi wa kuheshimiana, usawa, haki na ushirikiano wa kunufaishana, na kujenga jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja.

    Mkuu wa ujumbe wa China kwenye ofisi za Umoja wa Mataifa huko Geneva Balozi Chen Xu, amezitaka nchi mbalimbali ziimarishe ushirikiano wa kimataifa na kufuata taratibu za pande nyingi, ili kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili dunia na kuwanufaisha binadamu wote.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako