• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping wa China afanya mazungumzo na viongozi wapya wa Umoja wa Ulaya

    (GMT+08:00) 2020-06-23 09:38:01

    Rais Xi Jinping wa China jana tarehe 22 alifanya mazungumzo na mkuu wa Baraza la Ulaya Bw. Charles Michel na rais wa Halmashauri kuu ya Umoja wa Ulaya Bibi Ursula von der Leyen kwa njia ya video. Rais Xi amesema China inapenda kushirikiana na Umoja wa Ulaya na kuhimiza uhusiano kati ya pande hizo mbili kwenye kiwango cha juu zaidi baada ya maambukizi ya virusi vya corona. Hii ni mara ya kwanza kwa viongozi wa China na viongozi wa awamu mpya wa Umoja wa Ulaya kufanya mazungumzo.

    Rais Xi amesisitiza kuwa China na Umoja wa Ulaya zinapaswa kuzidisha maelewano na uaminifu, na kuwa nguvu mbili za kulinda amani na utulivu wa dunia na kuhimiza maendeleo na ustawi wa dunia, na pande hizo mbili zinapaswa kuunga mkono uzalishaji mali urudishwe kwa utaratibu.

    Habari nyingine zinasema rais Xi Jinping jana alituma barua ya pongezi kwa mkutano maalum wa vyama vya siasa vya China na nchi za Arabia, akieleza kuwa chama cha kikomunisti cha China CPC kiko tayari kuongeza mawasiliano ya kimkakati na vyama vya siasa vya nchi za Kiarabu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako