• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais mteule wa UNGA aahidi kujenga maafikiano na uaminifu kati ya nchi wanachama

    (GMT+08:00) 2020-06-23 17:01:28

    Rais mteule wa mkutano wa 75 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Bw. Volkan Bozkir amesema, atajitahidi kujenga maafikiano na uaminifu kati ya nchi wanachama wa Baraza hilo.

    Akizungumza katika mkutano usio rasmi wa Baraza hilo uliofanyika kwa njia ya video, Bozkir amesema atatoa umuhimu sawa kwa matarajio na maoni ya kila kundi duniani na wanachama wake, na kuongeza kuwa atatimiza wajibu wake kwa maslahi ya Umoja wa Mataifa na nchi wanachama wake.

    Kuhusu kanuni ya pande nyingi, rais mteule huyo amesema kanuni hiyo itaendelea kuwa ya ufanisi zaidi katika kutafuta suluhisho la changamoto mbalimbali duniani, na kwamba UNGA iko kwenye mwelekeo sahihi wa kuongoza juhudi hizo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako