• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wizara ya mambo ya nje ya China yazungumzia Mkutano 22 wa viongozi kati ya China na Umoja wa Ulaya

    (GMT+08:00) 2020-06-23 18:32:53

    Wizara ya mambo ya nje ya China leo hapa Beijing imefanya mkutano na waandishi wa habari ambapo mkurugenzi wa idara ya masuala ya Ulaya Bw. Wang Lutong amezungumzia mkutano wa viongozi wa China na Umoja wa Ulaya uliofanyika jana.

    Amesema viongozi wa pande hizo mbili wamebadilishana maoni kuhusu ushirikiano katika mapambano dhidi ya virusi vya Corona, ushirikiano wa uchumi na biashara na masuala mengine ya kimataifa na kikanda yanayofuatiliwa na pande hizo.

    Amesema matokeo muhimu ya mkutano huo ni pamoja na kuendeleza mazungumzo kuhusu mkataba wa uwekezaji kati ya China na Ulaya, kutangaza kuwa pande hizo mbili zitasaini mkataba wa alama za kijiografia kati ya China na Ulaya. Pande hizo pia zimefikia makubaliano juu ya masuala mengi ikiwemo kuunga mkono kanuni ya pande nyingi na biashara huria, kupinga vitendo vya upande mmoja na kujilinda kibiashara, kushirikiana kuhimiza ufufukaji wa uchumi duniani na kuhakikisha utulivu wa mnyororo wa uzalishaji na utoaji wa bidhaa duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako