• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa mazungumzo kati ya vyama vya siasa vya China na nchi za kiarabu wafanyika

    (GMT+08:00) 2020-06-24 09:22:24

    Mkutano wa mazungumzo kwa njia ya video kati ya vyama vya siasa vya China na nchi za kiarabu ulifanyika. Kauli mbiu ya mkutano huo ilikuwa "Kujenga jumuiya ya hatma ya pamoja kati ya China na nchi za kiarabu kwenye zama mpya", zaidi ya viongozi 60 wa vyama vya siasa vya nchi za kiarabu walishiriki kwenye mkutano huo wa siku tatu.

    Mkurugenzi wa Idara ya mawasiliano ya kimataifa ya kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China Bw. Song Tao, kwenye ufunguzi wa mkutano huo amesema Chama cha Kikomunisti cha China kinapenda kufanya juhudi pamoja na vyama vya siasa vya nchi za kiarabu kwa ajili ya kuhimiza ushirikiano, kuzidisha hali ya kuaminiana kimkakati, kukabiliana kwa pamoja na changamoto ya COVID-19, kulinda siasa ya pande nyingi na haki za kimataifa, na kusukuma mbele ujenzi wa jumuiya ya hatma ya pamoja kati ya pande hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako