• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bunge la Burundi lapitisha uteuzi wa makamu wa rais na waziri mkuu uliofanywa na rais mpya

    (GMT+08:00) 2020-06-24 09:23:10

    Bunge la Burundi limepitisha uteuzi wa makamu wa rais na waziri mkuu uliofanywa na rais Evariste Ndayishimiye, aliyeapishwa Alhamisi iliyopita.

    Mwanachama wa Chama cha upinzani cha UPRONA Bw. Prosper Bazombanza, ambaye aliwahi kuwa makamu wa kwanza wa rais mwaka 2014 hadi 2015, ameteuliwa kuwa makamu wa rais pekee kwenye serikali mpya kutokana na katiba iliyorekebishwa mwaka 2018.

    Katiba mpya ya Burundi imeweka wadhifa wa waziri mkuu, na kupunguza idadi ya makamu wa rais kutoka wawili hadi mmoja, na pia inaagiza kuwa waziri mkuu atateuliwa kutoka chama tawala, na makamu wa rais anatoka chama tofauti.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako