• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kaunti za mashinani Kenya zawa eneo muhimu kwenye mapambano dhidi ya virusi vya Corona

    (GMT+08:00) 2020-06-24 09:38:40

    Wakati Kenya ikiendelea kushuhudia ongezeko la watu walioambukizwa virusi vya Corona, kaunti za nje ya mji wa Nairobi zimekuwa ni maeneo yenye ongezeko la kasi la maambukizi ya virusi vya Corona ambako virusi hivyo vinaenea kwa kasi.

    Mji wa Mombasa ambao ni kitovu cha utalii Kenya ndio wenye maambukizi mengi zaidi. Hadi sasa mji huo umerekodi maambukizi 1,309 na idadi inaendelea kuongezeka. Ongezeko hilo linatokana shughuli za bandari ya Mombasa.

    Kati ya kaunti 47, kaunti 40 zimetajwa kuwa na maambukizi na wizara ya Afya ya Kenya imesema maambukizi hayo yataendelea kuongezeka.

    Kaunti za Kajiado, Busia, Migori na Mombasa ndio sehemu zenye maambukizi mengi, na wengi wa walioambukizwa hawana dalili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako