• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jukwaa la mawasiliano la bara la Afrika kutoa miongozo ya kupambana na COVID-19 kwa watu milioni 600

    (GMT+08:00) 2020-06-24 09:39:00

    Jukwaa la mawasiliano kuhusu afya lililozinduliwa jana kwa ushirikiano kati ya Kamati ya uchumi wa Afrika ya Umoja wa Mataifa ECA na kituo cha kuzuia na kupambana na maradhi cha Afrika (Africa CDC) na mashirika makubwa ya mawasiliano ya simu barani Afrika, linatarajiwa kutoa habari mpya kuhusu ushauri wa afya ya umma, hasa kuhusu mlipuko wa wa virusi vya Corona unaoendelea.

    Kwa mujibu wa ECA jukwaa hilo la simu za mkononi litatoa taarifa kwa vikosi kazi vya kitaifa na kikanda vya kupambana na virusi vya Corona, kwa ajili ya data za utafiti na hatua zinazoweza kuchukuliwa kiafya na kiuchumi.

    Kwenye hatua ya kwanza iliyoanza jumanne, jukwaa hilo litawafikia watumiaji wa simu za mkononi kwenye nchi 23 za Afrika, ikiwa ni asilimia 80 ya watumiaji wa simu za mkononi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako