• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mjumbe wa UM atahadharisha juu ya athari ya COVID-19 kwa mfumo wa afya Sudan Kusini

    (GMT+08:00) 2020-06-24 09:51:47

    Mjumbe wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia mambo ya Sudan Kusini Bw. David Shearer ametoa wito wa kufuatiliwa kwa athari inayowezekana kusababishwa na COVID-19 kwa mfumo wa afya nchini humo ambao umekuwa dhaifu tayari.

    Bw. Shearer amesema hayo kwenye mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya Sudan Kusini. Amesema hivi sasa wasiwasi mkubwa ni athari inayowezekana kusababishwa na COVID-19 kwa mfumo wa afya ulio dhaifu nchini humo, kwani kusimamishwa kwa utoaji wa chanjo, huduma za afya kwa mama, na matibabu ya kawaida kwa magonjwa yanayotibika kama vile Malaria, kuhara na nimonia kutasababisha ongezeko kubwa la vifo, ambavyo vitakuwa vingi zaidi kuliko vile vinavyosababishwa na COVID-19 moja kwa moja.

    Bw. Shearer amesema athari za ugonjwa huo zimeanza tu nchini Sudan Kusini, japo maambukizi 1,200 yaliyorekodiwa ni ya chini, lakini upimaji mdogo na unyanyapaa wa kijamii umeficha ukweli wa maambukizi ya virusi vya Corona.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako