• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mjumbe wa kudumu wa China UN atangaza China itachangia fedha na vifaa kwa UNRWA

    (GMT+08:00) 2020-06-24 10:03:34

    Mjumbe wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Zhang Jun ametangaza kuwa China itatoa mchango wa fedha na vifaa kwa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA).

    Balozi Zhang ametangaza kuwa mwaka huu China itatoa dola milioni 1 za Kimarekani kwa UNRWA, itatoa vifaa tiba vya kupambana na COVID-19 kwa idara za afya za UNRWA, na pia kutoa vifaa vya kujikinga kwa wakimbizi wa kipalestina walioko Palestina, Jordan, Lebanon na Syria kupitia UNRWA.

    China imeipongeza UNRWA kwa kutoa huduma muhimu na maalumu kwa wakimbizi wa kipalestina katika miaka iliyopita. Katika miezi kadhaa iliyopita, China imetoa msaada mkubwa wa matibabu kwa watu wa Palestina, na kuchangia uzoefu kuhusu kinga na tiba ya COVID-19.

    Bw. Zhang amesisitiza kuwa China inaunga mkono kithabiti haki halali za waplestina na itashirikiana na pande zote kutimiza amani ya kudumu katika eneo la Mashariki ya Kati.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako