• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda yafanya vipimo vya COVID-19 kwa wazee na wagonjwa katika maeneo yaliyoathiriwa zaidi na virusi hivyo

    (GMT+08:00) 2020-06-24 15:53:57

    Wizara ya Afya nchini Rwanda imezindua mpango wa kuwapima virusi vya Corona wazee wenye umri wa zaidi ya miaka 60 na watu wenye magonjwa sugu kama kisukari na magonjwa ya mfumo wa hewa katika wilaya ya Rusizi magharibi mwa nchi hiyo.

    Eneo hilo ambalo liko katika mpaka kati ya Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ni moja ya maeneo matatu nchini Rwanda ambayo yameripoti kesi mpya za virusi hivyo, na sehemu ya wilaya hiyo imefungwa kuanzia tarehe 4 mwezi huu.

    Wizara ya afya imeweka maabara ya kufanyia vipimo katika wilaya ya Rusizi ili kuhakikisha majibu ya haraka ya vipimo hivyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako