Nchi nyingi za Umoja wa Ulaya zimepunguza udhibiti wa maeneo ya mipaka, na kuanzia tarehe Mosi mwezi ujao, Umoja huo utafungua mipaka yake kwa baadhi ya wasafiri wa nje isipokuwa wanaotoka Marekani.
Hivi sasa, maofisa wa Umoja huo wanajadiliana kuhusu usalama wa wasafiri wanaoingia kutoka nje. Pia Umoja huo umesema, hautaruhusu watu kutoka Marekani kuingia katika nchi wanachama wa Umoja huo kutokana na idadi kubwa ya vifo vinavyotokana na maambukizi ya virusi vya Corona nchini Marekani.
Watu kutoka Brazil, Mexico na India pia huenda wakazuiliwa.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |