• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mfumo wa kuchukua hatua katika sehemu zenye maambukizi zaidi ni mwelekeo wa kukabiliana na maambukizi katika siku za usoni

    (GMT+08:00) 2020-06-24 16:48:30

    Tangu Beijing kutangaza maambukizi mapya ya virusi vya Corona Juni 12, pande mbalimbali zinafuatilia sana hali ya maambukizi mjini Beijing. Tarehe 19 mwezi huu, Gazeti la New York Times la Marekani lilitoa makala inayoeleza njia zinazotumiwa na Beijing kukabiliana na maambukizi hayo, na kusema kuwa Beijing imechukua hatua kwa haraka ili kuzuia mlipuko mkubwa wa maambukizi hayo.

    Gazeti hilo linasema, wakati maambukizi mapya yalipotokea Beijing, serikali ya mji huo ilichukua hatua mara moja, kufunga soko la mazao ya kilimo la Xinfadi, na kuchukua hatua za kuwaweka karantini watu wanaoishi katika majengo zaidi 40 karibu na soko hilo.

    Ingawa idadi ya maambukizi imefikia 249 mpaka tarehe 22, Beijing haikuchukua hatua za kufunga mji wote, kwani maduka ya kawaida, maduka makubwa, migahawa na sehemu nyingine zinaendelea na shughuli zao.

    Gazeti hilo linasema hali hiyo inatokana na uzoefu mkubwa uliopatikana na serikali ya China katika miezi kadhaa iliyopita. Kama njia hiyo ya kuchukua hatua katika sehemu zenye maambukizi mengi zaidi ikifanikiwa, mbinu kama hiyo huenda itatumiwa katika kukabiliana na maambukizi katika siku za usoni.

    Gazeti la South China Morning Post la Hong Kong linasema, wakati nchi za Asia zikianza tena shughuli za uchumi, zinakabiliana na hatari za kutokea tena kwa maambukizi ya virusi vya Corona, na njia iliyochukuliwa na Beijing inatoa mfano kwa nchi hizo. Ingawa changamoto bado zipo, lakini kutokana na kuwa kila mtu anachukua tahadhari, mfumo wa afya pia umefanya maandalizi ya kutosha kwa ajili ya kutokea tena kwa maambukizi. Maambukizi hayo ya virusi vya Corona katika mji wa Beijing hayatakuwa makubwa kama yalivyokuwa katika mji wa Wuhan, miezi kadhaa iliyopita.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako