• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uwezo wa upimaji wa virusi vya Corona nchini China umeongezeka na kufikia zaidi ya watu milioni 3 kwa siku

    (GMT+08:00) 2020-06-24 18:14:06

    Ofisa wa Kamati ya Afya ya China Guo Yanhong leo amesema, kwa sasa China inaweza kufanya upimaji wa virusi vya Corona kwa watu milioni 3.78 kwa siku, ikiwa ni ongezeko la asilimia 200 kuliko mwezi Machi.

    Hadi kufikia Jumatatu wiki hii, idadi ya jumla ya vipimo vya virusi vya Corona kote nchini China imefikia milioni 90.41, na idadi ya jumla ya vituo vya upimaji wa virusi vya Corona imeongezeka kutoka 2,081 mwanzoni mwa Machi hadi 4,804 ya sasa, ambayo ni ongezeko la asilimia 131.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako