• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wizara ya mambo ya nje ya China yasema "uhuru wa habari" unaotajwa na Marekani ni "vigezo viwili" na kitendo cha umwamba

    (GMT+08:00) 2020-06-25 08:34:44

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Zhao Zhijian amesema, kitendo cha Marekani cha kuviorodhesha vyombo vinne vingine vya habari vya China kuwa "mashirika ya kibalozi", ni hatua nyingine tena ya kukandamiza kisiasa vyombo vya habari vya China, ambayo imeonesha wazi kuwa kile Marekani inachokiita "uhuru wa habari" ni mazoea ya kutumia vigezo viwili na kitendo cha umwamba.

    Bw. Zhao ameitaka Marekani isitishe ukandamizi wa kisiasa na vikwazo visivyo vya haki dhidi ya vyombo vya habari vya China, na irekebishe makosa yake, la sivyo, China italazimika kuijibu kwa hatua za haki na lazima. Marekani tarehe 22 iliiweka televisheni ya China CCTV, Shirika la habari la China China News, Gazeti la Renminribao na Gazeti la Global Times kuwa "mashirika ya kibalozi."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako