• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nchi za Afrika zatakiwa kushiriki kwenye juhudi za kuhakikisha chanjo ya COVID-19 inapatikana

    (GMT+08:00) 2020-06-25 08:55:04

    Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini akiwa ni mwenyekiti ya zamu wa Umoja wa Afrika, amezitaka nchi za Afrika kushiriki kwenye juhudi za kuhakikisha chanjo ya COVID-19 inapatikana.

    Akiongea kwenye mkutano wa njia ya video kuhusu mchango wa uongozi wa Afrika kwenye utengenezaji na upatikanaji wa chanjo ya COVID-19, Rais Ramaphosa amesema viongozi wa nchi za Afrika wanatakiwa kuungana na kufanya mazungumzo na wahisani duniani kuchangisha fedha, na kukusanya fedha ndani ya bara la Afrika ili kuhakikisha upatikanaji mapema wa chanjo.

    Amesema ni muhimu kuwepo kwa utengenezaji mkubwa wa chanjo barani Afrika. Amesema sehemu ya chanjo za Muungano wa Kimataifa wa Chanjo GAVI, ikiwa ni pamoja na chanjo ya COVID-19 na zile kwa ajili ya mpango mpana wa utoaji chanjo, zinatakiwa kutengenezwa Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako