• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatoa vifaa tiba kuisaidia Zambia kukabiliana na COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-06-25 09:02:35

    Ubalozi na kampuni za China nchini Zambia wamechangia vifaa tiba kusaidia nchi hiyo kupambana na janga la COVID-19.

    Vifaa hivyo vikiwemo meza za kufanyia upasuaji, barakoa, dawa za kuua virusi na vifaa vya kujikinga (PPE) vimetolewa kwa hospitali ya mafunzo ya Chuo Kikuu cha Levy Mwanawasa ambayo inasimamia vituo viwili vya karantini.

    Konsela wa uchumi na biashara wa ubalozi wa China Bw. Ouyang Daobing, amesema kama nchi nyingine, Zambia pia imeathiriwa na janga la COVID-19, na China imetoa vifaa hivyo kuitika wito wa nchi hiyo wa misaada ya kupambana na janga hilo. Amesisitiza kuwa janga hilo bado linaendelea, hivyo juhudi za kukabiliana nalo haziwezi kulegezwa.

    Katibu mkuu wa Wizara ya Afya ya Zambia Bibi Kakulubelwa Mulalelo ameishukuru China kwa msaada huo, na kusema China si kama tu imetoa misaada wa matibabu, bali pia imetoa misaada katika sekta za miundombinu na mafunzo nchini Zambia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako