• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mawaziri wa mambo ya nje wa Misri na Marekani wafanya mazungumzo

    (GMT+08:00) 2020-06-25 16:35:01

    Waziri wa mambo ya nje wa Misri Sameh Shoukry na mwenzake wa Marekani Mike Pompeo wamefanya mazungumzo kwa njia ya simu na kujadili ujenzi wa Bwawa la GERD unaofanywa na Ethiopia katika Mto Nile na masuala mengine ya kikanda.

    Taarifa iliyotolewa na msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri Ahmed Hafez imesema, waziri Shoukry alizungumzia maendeleo yaliyofikiwa katika ujenzi wa Bwawa hilo kutokana na kusimama kwa majadiliano kutokana na msimamo wa Ethiopia.

    Amesema viongozi hao pia walizungumzia masuala mengine yanayogusa maslahi ya pande hizo mbili, ikiwemo hali ya sasa katika nchi za Libya, Syria, na Yemen.

    Mazungumzo kati ya viongozi hayo yamefanyika siku moja baada ya mawaziri wa mambo ya nje wa nchi za Kiarabu kueleza kuunga mkono msimamo wa Misri kuhusu suala la Bwawa hilo, ikiwa ni baada ya kufanyika mkutano kwa njia ya video ulioitishwa na Umoja wa Nchi za Kiarabu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako