• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa zamani wa Msumbiji asisitiza kuwa China imeiunga mkono nchi hiyo ilipokabiliwa na changamoto

    (GMT+08:00) 2020-06-25 16:48:04

    Leo tarehe 25 Juni ni Siku ya Maadhimisho ya miaka 45 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kibalozi kati ya China na Msumbiji. Rais wa zamani wa Msumbiji Bw. Joaquim Alberto Chissano alipoongea na waandishi wa habari wa CMG amesema, urafiki kati ya pande hizo mbili una historia ndefu, na ushirikiano kati ya nchi hizo mbili umepata mafanikio mazuri katika sekta mbalimbali zikiwemo uchumi, biashara na maisha ya wananchi. Amesema wakati Msumbiji ilipokabiliwa na changamoto, China ilikuwa tayari kuiunga mkono.

    Urafiki kati ya China na Msumbiji una historia ndefu. Rais wa zamani wa Msumbiji Bw. Joaquim Chissano amesema, tangu Msumbiji ilipofanya mapambano ya uhuru wa kikabila katika karne iliyopita, nchi hizo mbili zimekuwa zikisaidiana, na kuwa rafiki na ndugu wa kweli. Anasema:

    "Wakati Msumbiji ilipopambana na ukoloni, marafiki wa China waliiunga mkono. Tarehe 25 Juni mwaka 1975, marafiki wa China walishuhudia uhuru wa Msumbiji, na China ni moja kati ya nchi zisizo za Afrika ambayo ilianzisha uhusiano wa kibalozi na Msumbiji mapema zaidi duniani."

    Akizungumzia kuhusu mlipuko wa maambukizi ya virusi vya Corona nchini Msumbiji, Bw. Chissano amesema, China imekuwa ikiisaidia Msumbiji katika kupambana na maambukizi ya virusi tangu kesi ya kwanza iliporipotiwa. Anasema:

    "Hivi sasa China pia imeonesha uwajibikaji wake wakati wa kukabiliana na janga la virusi vya Corona. Si kama tu inatoa vifaa na misaada ya kupambana dhidi ya maambukizi ya virusi hivyo, pia imefanya juhudi kubadilishana uzoefu ulioupata kwenye mapambano hayo, ambao unachangia sana katika mapambano ya Msumbiji dhidi ya maambukizi hayo."

    Msumbiji iliwahi kuwa kituo muhimu kwenye "Njia ya Hariri Baharini" wakati wa enzi ya kale, na hivi sasa vilevile ni moja kati ya nchi za Afrika zilizojiunga na pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" la China. Bw. Chissano amesema, Msumbiji inanufaika kutokana na pendekezo hilo ambalo linatoa fursa kwa dunia kunufaika na fursa za kujiendeleza kwa pamoja na China, na kupata mustakabali mzuri. Anasema:

    "Hivi sasa Msumbiji inafanya juhudi za katika ujenzi wa Pendekezo la 'Ukanda Mmoja, Njia Moja' ambalo linazishirikisha nchi nyingi ikiwemo Afrika. Kama viongozi wa China walivyosema, 'Ukanda Mmoja, Njia Moja' inatoka kwa China, lakini inanufaisha dunia. Hili ni pendekezo linaloleta ushirikiano utakaozinufaisha nchi zote duniani. Msumbiji ikiwa nchi iliyoko kwenye kituo muhimu cha usambazaji wa bidhaa kwenye kanda hiyo, vilevile itakuwa nchi muhimu kwenye 'Ukanda Mmoja, Njia Moja'."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako