• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Viongozi wa China na Uholanzi wapongezana kwa kuzaliwa Panda

    (GMT+08:00) 2020-06-25 18:09:22

    Rais Xi Jinping wa China na mkewe Peng Liyuan wamebadilishana salamu za pongezi na Mfalme wa Uholanzi Willem-Alexander na Malkia Maxima kufuatia kuzaliwa kwa mtoto wa Panda nchini humo.

    Rais Xi na Mama Peng wamesema katika barua yao kuwa kuzaliwa kwa Panda huyo mwezi Mei katika Hifadhi ya Wanyama nchini Uholanzi ni furaha kubwa.

    Pia wamesema, tangu kutokea kwa janga la mlipuko wa virusi vya Corona, serikali na watu wa nchi hizo mbili wamesaidiana na kuandika historia nzuri ya urafiki ya kusaidiana katika shida na raha.

    Kwa upande wao, Mfalme na Malkia wa Uholanzi wamesema wamefurahishwa sana na kuzaliwa kwa Panda huyo. Pia wamesema, maisha hayo mapya sio tu ni ishara ya urafiki mwema kati ya nchi hizo mbili, bali pia ni mchango katika ulinzi wa uhai wa viumbe duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako