• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yazindua kituo cha kupiga simu kwa ajili ya wahudumu wa afya

    (GMT+08:00) 2020-06-26 08:39:37

    Kenya imezindua kituo cha uungaji mkono wa kisaikolojia kwa wahudumu wa matibabu walio mstari wa mbele.

    Waziri wa teknolojia ya habari na mawasiliano ya Kenya Bw. Joe Mucheru amesema kituo hicho kitasaidia kupata habari na kuchangia uzoefu kati ya wahudumu wa afya. Bw. Mucheru pia amesema kituo hicho kitatumika kama sehemu ya kutoa taarifa zote kuhusu COVID-19 kwa umma, na watashirikiana na mamlaka ya teknolojia ya Konza kutoa uungaji mkono wa kiufundi, miundo mbinu ya kuaminika na vifaa ya kutumia.

    Katibu tawala wa wizara ya afya ya Kenya Bibi Mercy Mwangangi amesema serikali inapenda kutumia majukwaa ya kidigitali kuimarisha mwitikio wa kupambana na virusi vya Corona.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako