• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jumuiya ya Nchi za Kiarabu yaunga mkono sera za mpito za Sudan

    (GMT+08:00) 2020-06-26 09:01:40

    Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu Bw. Ahmed Aboul-Gheit amesema jumuiya hiyo inaunga mkono Sudan wakati wa mpito wa nchi hiyo.

    Bw. Aboul-Gheit amesema hayo kwenye mkutano wa kimataifauliofanyikwa kwa njia ya internet kuhusu Sudan, na kufadhiliwa na Ujerumani, Umoja wa Mataifa na Umoja wa Ulaya. Waziri mkuu wa Sudan Bw. Abdalla Hamdok alishiriki kwenye mkutano huo.

    Bw. Aboul-Gheit amesisitiza tena ahadi za jumuiya hiyo kuhusu kutoa misaada zaidi kwa Sudan katika sekta za ujenzi, teknolojia na uchaguzi, na kutoa msaada wa fedha kwa maendeleo na miradi ya kibinadamu katika jimbo la Darfur na sehemu nyingine nchini humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako