• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kituo cha simu za dharura kuongeza uwezo wa mwitikio dhidi ya COVID-19 nchini Somalia

    (GMT+08:00) 2020-06-26 09:18:13

    Umoja wa Mataifa umesema kituo cha simu za dharura kilichozinduliwa hivi karibuni nchini Somalia kimehimiza mwitikio wa afya kwenye mapambano dhidi ya COVID-19.

    Kituo hicho kinachoungwa mkono na Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) kinapokea zaidi ya simu 8,000 kila siku kutoka wanaojisikia wagonjwa au wanaohitaji ushauri kuhusu COVID-19 nchini Somalia.

    Watu wanaotafuta ushauri kuhusu COVID-19 wanapaswa kupiga simu 449, ambayo ni simu ya bure iliyowekwa na serikali ili kutoa ufikiaji wa haraka kwa msaada wa matibabu ya dharura.

    Habari nyingine kutoka Kituo cha Udhitibi na Kinga ya Maradhi barani Afrika (Africa CDC), zinasema hadi jana alasiri idadi ya maambukizi ya COVID-19 barani Afrika imefikia 336,019.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako